Serikali ya Marekani imetangaza kutuma askari wengine elfu moja na miatano nchini Iraq kwa minajili ya kukabiliana na magaidi wa Daesh.
Marekani imesema kuwa inawatuma askari hawa kuungana na askari wengine walioko Iraq kwa ajili ya kutoa ushauri na mafunzo kwa jeshi la Iraq ili waweze kukabiliana na magaidi hao.
Josh Earnest, mzungumzaji wa ikulu ya Marekani aliongeza kwa kusema kuwa hatutumi askari hawa kwa minajili ya kwenda mstari wa mbele kupambana bali kwenda kutoa mafunzo ya ustadi wa kupamabana.
Magaidi wa Daesh wamekuwa ni tishio kubwa kwa amani na uwepo wa serikali ya Syria na Iraq, na wamedhibiti baadhi ya sehemu za nchi hizo na kuweka kambi zao.
8 Novemba 2014 - 07:42
Msimbo wa Habari: 649902
Serikali ya Marekani imetangaza kutuma askari wengine elfu moja na miatano nchini Iraq kwa minajili ya kukabiliana na magaidi wa Daesh.